AZMA FEAT KITA & CANT DIDAS - UTATA WA KATIBA VIDEO AND LYRICS

KABLA HAMJAJIULIZA wangapi wanataka serikali tatu?,
wangapi mnataka serikali mbili?, wangapi wanataka serikali moja? Msisahau KUJIULIZA ni wangapi hatutaki serikali

Verse 1.
Wananchi wengi tuna shida ya njaa kali,
hatuna shida ya serakali za serikali,
Tunahitaji kunufaika kwa rasilimali,
msituhimize juu ya ujasiriamali,
wakati nyinyi mnawekeza kwenye politics,
itakuwa ni politrix, zenye poli fix,
wanasiasa mnatupotosha, nikitazama kwa jicho la 3,
sioni haja ya serikali 3, hizi mbili zilizopo ni mzigo tosha,
ukiacha hili la Muungano, kuna mengi yenye tija kwa Watanzania,
yanaacha yanafumbiwa macho, wanang'ang'ana na muungano,
naona gape la wenye nacho na wasio nacho linazidi kuongeza,
wasio nacho wanazidi kumegeka,
Tangu nazaliwa sikuikuta Tanganyika,nilikuta TANZANIA,
sitadanganyika,nikaanzisha taasisi za kuiua TANZANIA,
iliyoanzishwa na waasisi JK NYERERE NA KARUME,
TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA........
NB
SHARE HUU WIMBO KWA WATANZANIA WOTE WANAO IPENDA NA KUITAKIA MEMA TANZANIA YETU,NA WANAOHESHIMU NA KUILINDA AMANI TULIYO NAYO NA KUUENZI MUUNGANO WETU....

Taifa moja,nchi moja, serikali moja......

HUO NDIO MUUNGANO WA KWELI.....

Comments